March 4, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Al Masry kimewasili asubuhi ya leo nchini kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Simba SC utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumatano ya wiki kesho.

Al Masry wametua nchini na kupokelewa na basi la Azam FC ambalo liliwapeleka moja kwa moja katika hoteli waliyopanga kufikia.



Waarabu hao walifuzu kuendelea na mashindani hayo baada ya kuwafunga Wazambia, Green Buffaloes kwa mabao 5-2.

Mchezo wao dhidi ya Simba SC utachezwa Jumatano ya Machi 7 2018, majira ya saa 12:00 jioni.




1 COMMENTS:

  1. Naona ni jambo zuri kwa wageni kukaribishwa vizuri na kupokelewa na basi la Azam, ni basi zuri luxury na wageni watatupa heshima. Lakini isije ikaonekana ni dhambi siku basi la Simba likatumika kuipokea timu ngeni itayokuja kucheza na Azam kwenye mashindano haya. Vizuri tuhalalishe jambo hili lisije likawa la upande mmoja tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic