March 20, 2018


Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Yanga, Hussein Nyika, amesema hawaiogopi timu yoyote watakayopangwa nayo katika Kombe la Shirikisho Afrika kesho.

Droo hiyo ambayo inataraji kufanyika kesho mchana, itahusisha timu zilizoanguka kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika, na zilizo kwenye Kombe la Shirikisho.

Nyika ameeleza kuwa wao wapo tayari kupambana na yeyote yule ambaye watapangwa naye, kwakuwa watafanya maandalizi ya kutosha.

Akizungumza na kipindi cha michezo kupitia Radio One, Nyika anaamini katika mpira matokeo yoyote yanaweza kutokea ndani ya dakika 90, lakini watajipanga kurekebisha makosa yaliyotokea Ligi ya Mabingwa Afrika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic