NI PIGO KWA AZAM, AMOAH KUSAFIRISHWA AFRIKA KUSINI KUTIBIWA GOTI
Afisa Habari wa klabu ya Azam FC, Jaffer Idd Maganga, amesema kuwa Mshambuliaji wao, Mghana, Daniel Amoah, atasafirishwa kuelekea Afrika Kusini kupata matibabu.
Amoah atasafirishwa nchini humo kutokana na maumivu ya goti ili kutibiwa ili baadate aweze kurejea kikosini kujiunga na wenzake.
Maganga ameeleza kuwa mchezaji huyo ataondoka siku chache zijazo kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kutibiwa goti hilo.
Azam FC ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Ligi Kuu Bara hivi sasa, nyuma ya Yanga na Simba zilizo juu yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment