March 20, 2018


Mchezaji wa zamani wa Yanga, Bakali Malima 'Jembe Ulaya', amesema haipi nafasi Yanga ya kufanya vizuri katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga imeangukia kwenye michuano hiyo baada ya kuondolewa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers kwa mabao 2-1.

Akizungumza na kipindi cha michezo kupitia Radio One, Malima amesema haoni nafasi ya Yanga kusonga mbele kutokana na vigogo waliopo kwenye mashindano hayo.

Baadhi ya timu kongwe na kubwa zilizopo ni Enyimba FC, Raja Cassablanca na USM Algier na Al Masry SC iliyowatoa Simba.

Droo ya upangaji wa timu zitakazokutana kwenye mashindano hayo inataraji kufanyika kesho Jumatano mjini Cairo Misri.

2 COMMENTS:

  1. Namuomba Mwenyezi Mungu Yanga ipangiwe timu ya Al Masry

    ReplyDelete
  2. Hakuna kitu kibaya duniani kama kukariri! Na kukariri kubaya zaidi ni kukariri katika kushindwa na si kutafuta suluhisho.
    Kisha tutarajie maendeleo ama ushauri kwa wastaafu waliokata tamaa. Hatujiulizi Ethiopia tulikuwa tinawapiga 9-0 je leo ikoje hali?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic