March 27, 2018




Na George Mganga

Katibu Mkuu wa zamani wa Simba, Seif Kaduguda, amekumbushia Simba aliyoiona ni bora katika historia ya maisha yake tangu aanze kuipenda.

Kaduguda ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Simba chini ya Utawala wa Mwenyekiti, Hassan Dalali, amesema anaikumbuka Simba iliyowahi kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 1974.

Akizungumza na Radio EFM, Katibu huyo wa zamani amesema anaikumbuka Simba hiyo iliyokuwa na baadhi ya wachezaji kama Athumani Mabosasa (Golikipa ambaye ni Marehemu kwa sasa), Shaaban Baraza aliyekuwa anacheza beki namba mbili na Mohammed Kajoli aliyekuwa anacheza kama beki namba tano 'Full Back'.

Mbali na kuikumbuka Simba hiyo, Kaduguda amesema anakumbuka ushindi wa mwisho wa Simba dhidi ya Yanga katika msimu wa 2016/17 wa mabao 2-1, ulimfanya atembee kwa mguu kutoka Uwanja wa Taifa, Temeke Dar es Salaam mpaka Gongolamboto kutokana na furaha aliyoipata.

Katika mchezo huo, Simba ilijipatia mabao yake kupitia Laudit Mavugo aliyefungwa kwa njia ya kichwa akitengenezewa mpira na Kichuya, huku Kichuya naye akifunga bao la pili kwa mpira wa krosi aliopiga kushoto mwa Uwanja, na kumuacha aliyekuwa kipa wa Yanga, Deo Munish 'Dida'.

Bao la Yanga lilifungwa na Simon Msuva kwa njia ya penati, mapema kabisa kwenye dakika za mwanzo za mchezo baada ya Obrey Chirwa kuchezewa madhambi katika eneo la hatari.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic