Kiungo wa Simba raia wa Ghana, James Kotei amesema pamoja na timu yao kuonekana kupata shida ya kuwafunga Al Masry ya Misri, kwenye mchezo wao wa raundi ya kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, anaimani kubwa ya kung’oa kwao katika mchezo wa marudiano unaotarajiwa kuchezwa Machi 17, mwaka huu.
Kotei aliyejiunga na Simba, Julai 12 msimu wa 2016/17 amesema anaamini watapata ushindi katika mchezo wa pili kwa kuwa wameshajua mbinu zao na kwamba mapungufu waliyoyafanya kipindi cha kwanza kocha atayafanyia kazi.
“Natambua wazi kuwa Al Masry ni timu kubwa sana ukilinganisha na uwezo wetu katika rekodi za Afrika, lakini ukubwa wao siyo sababu pekee ya kutufanya sisi tukubali kuondolewa kwenye mashindano haya muhimu.
“Tumeshajua namna ya kupambana nao huko kwao ili tuweze kuwafunga na kuendelea katika hatua inayofuata, hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya kupambana kwani kila mmoja wetu anatambua kuwa hatuna mashindano mengi tukitolewa zaidi ya hayo na Ligi Kuu Bara,” alisema Kotei.
SOURCE: CHAMPIONI
Kila siku mnasema tumeshajua tumeshajua sasa fanyeni kweli. Anzisheni mashambulizi makali toka mwanzo wa mchezo. Mnarudisha sana nyuma mipira bila sababu hata kocha huwa anahamaki wakati mwingine mpira ushavuka nusu uwanja badala ya kupress kwenda mbele eti anrudishia beki hadi kwa golikipa Manula. Mnazidi kuuchelewesha mpira twende mbele kwa mbele toka dakika ya kwanza ya mchezo warabu tutawabandua tu.
ReplyDeleteHuyu jamaa mbona maneno yake ya ovyo na ikiwa yeye ni mpenzi wa yanga basi pia nao hutamka maneno kama hao na ni lugha inayotumika kotw duniani
ReplyDelete