KUSHINDWA KUPELEKA WANARIADHA SPAIN KWAIPONZA RT, TANZANIA KUPIGWA FAINI NA IAAF
Wakati Wanariadha wengi duniani wakiwasili huko Valencia, Spain kwa ajili ya Mashindano ya Makubwa ya Dunia ya Riadha Nusu Marathon, Tanzania imekosa mwakilishi.
Tanzania kabla ilikuwa iwakilishwe na Wanariadha tisa, kabla baadaye kukutana na ‘zengwe’ la wanariadha hao ambao ni watumishi wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), kuitwa kambini kwa ajili ya kwenda kwenye mafunzo ya kijeshi na baadaye kubaki wawili ambao wangewakilisha, nao wamegonga mwamba.
Kuafuatia kushindwa kusafiri kuelekea nchini humo, Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) linaweza kuipiga faini Tanzania baada ya kushindwa kupelekea wawakilishi.
Akizungumza na kipindi cha michezo kupitia Radio One, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday, amesema Tanzania inaweza kufungiwa kutokana na kwenda kinyume na taratibu za mashindano huku baada ya kukosa ruhusa ya wafanyakazi wanaotokea taasisi za kiserikali.
"Ni kweli tunaweza kufungiwa, tumeshindwa kupata ruhusa ya wafanyakazi wanaoshiriki mchezo huu kutoka serikalini, hivyo itatubidi tulipe"
0 COMMENTS:
Post a Comment