Ikiwa ni baada ya Yanga kufungwa huku Simba ikiambulia sare katika michuano ya kimataifa, Katibu wa Baraza la Wazee la Yanga, Ibrahim Akilimali amefunguka kuwa ni wazi timu hizo zimejiweka katika mazingira magumu ya kusonga mbele.
Yanga ilifungwa 2-1 na Township Rollers ya Botswana katika Ligi ya Mabingwa Afrika huku Simba ikitoka 2-2 dhidi ya Al Masry ya Misri katika Kombe la Shirikisho, michezo yote ikichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.
Akilimali alisema timu zetu kimataifa msimu huu hazikuwa na maandalizi, hivyo siyo rahisi kuweza kusonga mbele.
“Ukweli ni kwamba, timu zetu kwenye michuano ya kimataifa msimu huu zimeshindwa, ni vyema wakajipanga kwa ajili ya michuano hii mwakani na siyo kwa sasa.
“Sababu wote wamekutana na timu ambazo zina uwezo na zimejiandaa vyema ndiyo maana zikashindwa kupata matokeo hapa nyumbani na siyo rahisi wao kwenda kupata matokeo huko ugenini ni ngumu sana.
“Wanatakiwa kujipanga upya na kuangalia wapi wamekosea ili kuweza kurudi kwenye mstari lakini kusema watasonga mbele kwenye michuano hii siyo rahisi kabisa,” alisema Akilimali.
Mzee pambana na hali yako
ReplyDeleteKwa hiyo wasiende kwenye mechi za marudiano? Mbona mzee unakuwa negative tu kila wakati? Wape moyo vijana wakati mwingine ili isaidie kupambana kuliko kukata tamaa. Kwa nini hukushiriki kutoa ushauri wakati wa maandalizi unasema sasa ili iweje?
ReplyDeletetimu ya Township Rollers wachezaji wake hawadai mishahara kama hao wa Yanga na posho zao ni balaa sasa kama ewe unajiita ni katibu wa baraza lako la wazee wenzio una mpango gani wa utatua tatizo la mishahara na posho za wachezaji wako ili uweze kuamsha morali au domo tupu tu na bingwa wa kukosoa msaada/mchango wako kama katibu wa kudumu wa wazee katika klabu ya Yanga ni upi hasa?
ReplyDelete