March 9, 2018


Na George Mganga

Mshambuliaji wa Tottenham Hotspurs, Harry Kane, ameahidi kuendelea kusalia ndani ya klabu hiyo kwa zaidi ya msimu mmoja, licha ya kusalia kwake, uongozi wa Tottenham unapambana kumbakiza kikosini beki wake Toby Alderweireld pamoja na beki wa kushoto, Danny Rose, wanaowania na Manchester United. The Sun.

Kocha wa Chelsea, Antonio Conte, sasa anawaniwa na matajiri wa Ufaransa, PSG, ili achukue nafasi ya Unai Emery, ambaye inaarifiwa anaweza akaondoka mwishoni mwa msimu. Awali ilielezwa PSG wanataka kumsajili Arsene Wenger. L'Equipe - in French.


Uongozi wa Manchester United upo nyuma ya Kocha, Jose Mourinho, ambaye amesema atawauza wachezaji ambao hawaendani na falsafa yake ya uchezaji. Independent.

Chelsea na Real Madrid wako mbioni kuwania saini ya mshambuliaji Mpoland wa Bayern Munich, Robert Lewandowski (29) ambaye milango yake ya kuondoka ipo wazi katika msimu huu wa majira ya joto. Bleacher Report.

Chelsea vilevile inamnyatia beki Msenegal, Kalidou Koulibaly, anayekipiga huko Napoli, Italy. Arsenal na Manchester United zinatajwa pia kumsajili beki huyo. Star.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic