March 20, 2018




Kocha wa Simba, Pierre Lechantre yuko kwao nchini Ufaransa.

Lechantre yuko Ufaransa ambako amerejea akitokea jijini Cairo, Misri.

Aliondoka Cairo baada ya kufika jijini humo kutokea Port Said, akiwa na kikosi chake cha Simba kilichokuwa kimekwenda kuivaa Al Masry katika mechi ya pili ya Kombe la Shirikisho.

Simba imetolewa baada ya sare mbili za nyumbani na ugenini na Masry wamesonga mbele na faida ya mabao.

Lechantre amekwenda nyumbani kwao Ufaransa kutokana na matatizo ya kifamilia.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah au Try Again ameithibitishia Simba kwamba kocha huyo atarejea baada ya siku chache.

2 COMMENTS:

  1. Niwaombe simba waje na hadisi nyengine ya kubadirisha kocha wa muache amalize msimu

    ReplyDelete
  2. Sina ufahamu wa kutosha ni aina gani ya mchakato TFF inatumia katika kutafuta walimu wa timu ya Taifa. Ila Mtu akifanya jambo jema ni vyema kumpongeza. Mimi bado nashangazwa sana na klabu ya Simba kumuajiri yule Kocha wa kifaransa. Ni nani aliwapa dili la kumnasa? Na kama yupo kwanini asitumike kututafutia kocha wa timu ya Taifa? Kwani kumekuwepo na ubabaishaji mkubwa linapokuja suala la kuajiriwa kwa kocha wa timu ya Taifa. Ila Kwa mbali ninachokiamini mimi Mohamed Mo alimleta yule mzungu kwa hasira. Ndio hasira wakati mwengine ni tamu kuliko furaha. Kabla ya mechi ya marudiano kati Almasry na SIMBA kule port said. Nilipitia kuangalia baadhi ya vyombo vya habari vya michezo Egypt. Nikakutana na habari zinazozungumzia kauli ya kocha wa Almasry Bw Hossam. Aliulizwa anaionaje Simba? Akasema haitakuwa mechi rahisi hata kidogo. Na kubwa alilokuwa akihofu zaidi ni kocha wa Simba. Alimuelezea kuwa kocha huyo anauzoefu na mbinu zisizo za kawaida barani Africa. Na kweli wasi wasi wake kocha wa Almasry juu ya kocha wa Simba haukuwa wa bure, kwani amechoropoka kwenye tundu la sindano la sivyo kwa vurugu za mashabiki za Almasry angekuwa keshakimbia. Licha ya kipindi kifupi alichofanya kazi Simba mfaransa yule ameonesha kuwa ni kocha hasa. Hata vilabu kadhaa vya pale Misri Zimeshangazwa sana na Game technical Approach ya Simba walioinesha pale port said. Ni vigumu timu kwenda port said ikatoka salama hata akina Alhal wanachemsha pale wakati mwengine hadi damu kumwagika. Ningetamani uongozi wa Timu yetu ya Taifa ukjifunza kutoka SIMBA SC. Katika hili suala la kocha. Wazungu wanasema sometimes you can run out of chances when you stop taking them.
    kwangu mimi kuwepo kwa huyu kocha wa Simba nchini ni moja ya chance ambazo kama wadau wa soka tunatakiwa kujifunza. Na kwa mbinu hizi za mfaransa sina wasiwasi hata kidogo kama tuna mpa timu ya Taifa kwa hawa vijana tulionao sasa Afcon tunakwenda mapema tu. Mbinu za mfaransa ndio mbinu zinazozimaliza timu zetu tunapokutana na timu za ukanda wa kaskazini ya Africa na Magharibi. Ningependa kumuona mfaransa akiendelea mufundisha nchini wasiwasi wangu sidhani kama atadumu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic