March 10, 2018


Na George Mganga

Ligi Kuu England inaendelea tena Jumamosi ya leo kwa mechi kadhaa kupigwa, ambapo mechi inayosubiriwa kwa hamu ni ya Manchester United ambao wataikaribisha Liverpool pale Old Trafford.

Manchester United inaingia kucheza mchezo huu ikiwa na tofauti ya alama mbili mbele, dhidi ya Liverpool katika msimamo wa ligi.

Mpaka sasa Manchester ina ponti 62, na Liverpool ina 60 huku timu zote zinaingia kucheza mechi hii zikiwa zimecheza michezo sawa, michezo 21 ya ligi msimu huu.

Kuelekea mchezo huu, United inaikaribisha Liverpool Old Trafford ikiwa na rekodi mbaya ya kufungwa mechi 5 za ligi msimu huu, tofauti na Liverpool iliyopoteza 3 pekee.

Manchester imefunga jumla ya mabao 56 katika ligi, huku Liverpool ikiwa na zaidi ya United kwa kufunga mabao 67, hapo tunaona tofauti ni mabao 11.

Marouane Fellain anaweza akacheza mechi kuelekea kupona majera yake ya goti yaliyokuwa yanamsumbua, hali iliyosababisha kukosekana kwenye baadhi ya michezo ya ligi na hata UEFA Champions League.

Antonial Martial ana uwezekano wa kukosekana pia kwenye mchezo wa leo, huku Zlatan Ibrahimovic naye hatokuwepo sababu ya kusumbuliwa na goti pia.

Ander Herrera naye atakosekana kufutia majeraha ya nyama za paja, pamoja na Daley Blind ambaye pia ni majeruhi.

Liverpool wao wanaweza kuwa na Andrew Robertson, Jordan Henderson na Georginio Wijnaldum ambao hali zao kiafya zipo sawa baada ya kutoka majeruhini.

Mechi hii itaanza saa 9 na nusu kwa saa za Afrika Mashariki






0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic