March 10, 2018


Na George Mganga

Ukiachilia mbali watani wao wa jadi, Yanga, walio na nafasi pia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, Simba SC ndiyo timu iliyo na takwimu bora kuliko mpaka sasa.

Simba imecheza imecheza jumla ya michezo 20 ya ligi pamoja na Yanga, huku timu zingine zote zimeshacheza michezo 21.

Ukiangalia kwenye takwimu Simba inaongoza ligi kwa tofauti ya alama tatu dhidi ya watani wao, Yanga, walio na pointi 43 huku Simba ana 46.

Simba, Stand United, Mbao FC na Yanga ndizo timu pekee zilizoenda sare ya mechi saba (7) mpaka sasa, tangu msimu huu wa ligi (2017/2018) uanze.

Mbao na Stand wameungana wakongwe (Simba na Yanga) kwenye idadi ya mechi zilizoenda sare kuwa 7 kwa wote, ingawa zenyewe zimeshacheza michezo 21.

Katika jumla ya michezo 20 ambayo Simba imeshacheza, haijapoteza hata mmoja, Yanga ikipoteza mmoja na Azam akipoteza zaidi ya mmoja huku zingine zote zikipoteza zaidi ya miwili.

Simba wanarekodi nzuri ya mabao ya kufunga, mpaka hivi sasa wamefunga mabao 49 huku Yanga akifunga 35, ukiangalia utofauti hapo ni mabao 14 ambayo Yanga ameachwa.

Ukiangalia takwimu hizo, ni dhahiri shahiri Simba amewazidi wenzake, na kinachombeba ni kutokupoteza mchezo hata mmoja.

Bado watani hawa wawili, Simba na Yanga, kila mmoja ana nafasi ya kuchukua ubingwa endapo mmoja kati yao atateleza kwenye michezo iliyosalia kwenye ligi.


1 COMMENTS:

  1. there is no news worthiness in this article...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic