LIVERPOOL NI MOTO WA KUOTEA MBALI, YAILAZA NEWCASTLE 2-0, SALAH AWEKA REKODI HII
Majogoo wa Anfield wamezidi kuuwasha moto baada ya kuilaza Newcastle United kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu Uingereza uliopigwa usiku wa leo.
Alikuwa ni Mohamed Salah aliyeanza kucheka na nyavu za Newcastle kwa kutupia goli la kwanza kwenye dakika 40.
Sadio Mane naye alicheka na nyavu kwenye dakika ya 55 na kuufanya mchezo uwe mbele kwa Liverpool kwa mabao hayo mawili.
Matokeo yamewafanya Liverpool wapande juu ya msimamo wa ligi mpaka nafasi ya pili wakiwa na alama 60 juu ya manchester United iliyo na 59.
Na nyota Mmisri, Mohammed Salah ameweka rekodi ya kufunga mabao 32 katika mechi 29 za Ligi, sawa na idadi ya mabao waliyofunga Newscatle United msimu huu.
0 COMMENTS:
Post a Comment