MAHUNDI AIPA ALAMA TATU MUHIMU AZAM DHIDI YA SINGIDA, SASA YABAKIZA ALAMA MBILI KUIFIKIA YANGA
Na George Mganga
Kikosi cha Azam FC kimeutumia vema Uwanja wake wa nyumbani kwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida United.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Azam Complex, dakika 90 zilimazilikwa kwa kushuhudia bao moja pekee likiwekwa kimiani.
Mfungaji wa bao hilo alikuwa ni Joseph Mahundi aliyefunga katika dakika ya 16 ya kipindi cha kwanza
Matokeo hayo yanaiweka Azam kwenye nafasi ya 4 ya msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kufikisha alama 38 nyuma ya Yanga iliyo na 40.
0 COMMENTS:
Post a Comment