March 29, 2018







Kumjibu mtu mjinga ni kufanana nae..ila kumwelimisha mjinga ni kumsaidia


Nimeona hyo video ya Saleh Ally na mchezaji wa Baroka fc (Kama nimeiandika vema )ya nchini Afrika kusini Abdi Bhanda.


Bhanda alipata kuichezea klabu ya Simba kabla ya kujisajili na timu yake mpya.


Kwenye video hyo Bhanda anaulizwa swali na mwandishi ni kitu gani hutatamani kikutokee ktk career yako ya kucheza Soka.. akajibu.jambo nisilotaka kuja kuntokea ni kwa viongozi waliopewa dhamana kuchukua mamlaka ya kwenda kuongea na vyombo vya habari huku wao hawana mamlaka hayo..huku akikiri kuwa kuna watu wameajiriwa kwa kupewa hyo mamlaka..


Halaf akaendelea kwa kuponda kwa mfano wangu eti kulalamikia maamuzi ya refarii aliochezesha mchezo wetu wa Ligi kuu baina yetu na Yanga..mchezo ulioisha kwa sare ya bila kufungana..



Mchezaji huyo alienda mbali zaidi kwa kusema jambo hilo linasababisha mpira wetu usiende mbele..

Nimjuze kwanza wajibu wa kazi yangu..mm ndio msemaji rasmi wa klabu ya Simba na nimepewa hyo mamlaka kama alivyosema yy mwenyew ktk interview yake..nikiongea mm naongea kwa niaba ya kamati ya kamati ya utendaji wa Simba..siongei jambo ila uongozi umeridhia na ndio maana kwa kipindi chote ambacho nipo Simba haijatokea hata kwa bahati mbaya mm kupishana kauli na viongozi wenzangu..
Hvyo dogo aelewe ile ni mamlaka yangu.


Pili mm kwenda kulalamikia maamuzi yale ni stand ya klabu na sikukurupuka kama alivyokurupuka yy ambae hata hajui nani msemaji rasmi wa klabu ya Simba..nimwambie kuanguka kwa mpira kuna sababu nyingi nchini na sio kulalamikia waamuzi pekee..hata huko South unapoomba Mungu watu hulalamikia waamuzi na walalamikaji ni viongozi,mashabiki,makocha na hata wachezaji.


Pia asisahau kulalamika kwangu ndio kulimsaidia asifungiwe adhabu kubwa na TFF baada ya kumpiga George kavila wa Kagera Sugar,hali iliopelekea kupata fursa ya kucheza Cosafa cup ambapo akaonekana na kusajiliwa huko South..

Nimkumbushe pia kulalamika kwangu ndio kulikopelekea utetezi ktk shauri lake kwa uongozi wa Simba ambapo alikuwa afukuzwe timu kitambo kwa kukosa nidhamu na maadili ya kambi..tena nilifanya utetezi mbele ya Bi mkubwa wake na bwana Bosnia ambae ni kama mlezi wake
Na hapo sitaki kumkumbusha huo ulalamishi wangu ulivyomnusuru yy ktk lile shauri lake la jinai..

Nimalizie kwa kumwambia weka akiba dogo..bado hujafika kokote wala usijione ushakuwa Abedi Pele au Lucas Radebe..huwa nazisikia tambo zako mbalimbali ukihojiwa na media za Tanzania..wakati mwingine ukibeza hata ulipotoka!!


Sijui ungekuwa ww ndio Samata ingekuwaje?
Sijawahi kumsikia Samata kwa njia yoyote akiponda hadharani viongozi wa bongo wala Simon Msuva au Ulimwengu..ila ww uliohamishia mpira mdomoni..jifunze kwa waliokutangulia na ujiwekee malengo yako ili ww,familia yako na Taifa kwa ujumla wafaidike,kupambana na mtu mwenye taaluma ya kuongea na kuandika ni kututafuta muhali tukaja kuongea yasioandikika....

HAJI S MANARA

9 COMMENTS:

  1. Naona kaamsha popo mzee...angalau aangalie utofauti kati ya Afisa Habari na Msemaji

    ReplyDelete
  2. Vitu vingine sio habari

    ReplyDelete
  3. Kila binadamu ana haki kusema anachoona kinampendeza ili mradi havunji sheria za mamlaka husika.Sioni kosa la Banda kwa kusema yanayompendeza au yanayomkera lkn pia kwa ushauri wa bure kwake Banda ni vizuri ukaweka akiba ya maneno,na kuangalia mienendo ya kaka zako kina Samatta, Ulimwengu, Msuva ili maisha yaendelee.

    ReplyDelete
  4. Myonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Manara kwa kiasi kikubwa katika hili la Banda yupo sahihi kabisa. Banda anatakiwa kufocas zaidi na kule anapotaka kwenda aache blah blah. Banda aelewe kabisa yakwamba yeye bado ni mwanafunzi hajawa mwalimu bado kwani kama kweli anania ya kufika mbali basi aliyoyaona na aliyokutana nayo na anyokutana nayo ni mwanzo tu wa safari haina haja ya yeye kukoment kitu chochote kwani bado yupo safarini asubiri atakupofika ndio asimulie pengine anatakiwa kutafuta dairy au daftari la kumbu kumbu aandike kila anchokiona na kusikia na vinavyomkuta kuliko kuropokwa hovyo maneno yake yaweza kuja kua kiunua mgongo chake kwa kuja kuandika nakala ya kitabu akauza. Sasa kama Banda hakiba yake ya stori anairopokea hovyo sasa nani atakuja kuwa na hamu yakuja kumjua kiundani nani Abdi Banda? Wakati mwengine vijana wanahitaji wasimamizi wa kuwaongoza jinsi gani ya kujilinda kama professional kwani hadhi ya kuwa mtu star ni ile hali ya muhusika kujichunga kikauli na vitendo vya hovyo.wasukuma wanasema...It is nice to be important,but it is more important to be nice.

    ReplyDelete
  5. Banda ni kipaji halisi miongoni mwa vijana wa kitanzania katika masuala ya soka. Binaadamu kuteleza ni jambo la kawaida ila waandishi wa habari nao wawe na hekima ya kuwaepusha vijana na kauli tata. Nilitegemea kusikia Banda akizungumzia zaidi masuala ya Gym nakadhalika yanayohusiana na maendeleo yake ya mpira. Banda anakimo kizuri kwa nafasi yake ya ulinzi wa kati lakini anatakiwa kuingia vitani na Gym na kuekeza katika mipangilio ya mlo sahihi ili kulijaza umbo lake kimazoezi kitu amabacho kitamuongezea thamani kutokana na ukweli ni kwamba umbo liloshiba kwa central defender ni moja kati ya sifa wanzozitafuta wazungu. Hayo mengine yote ya uswahilini,Banda anatakiwa kuwaachia waswahili wenyewe.

    ReplyDelete
  6. Huyu manara vipi! Hivi ni mwanaume au mwanamke maana kama mwanaume why hana sifa ziada za mwanaume za kuwa na kifua, why kila cku yeye tu anabore

    ReplyDelete
  7. Hawa akina manara ndyo wa kufungiwa soka maisha maana anaendekeza marumbano na mipasho badala ya kupromote soka. Msemaji wa club ni zaidi ya kuwa mropokaji na kasuku. Au manara ni msemaji wa kilabu cha pombe?

    ReplyDelete
  8. Banda mchezaji mzuri ila anakosea na anapenda sana kulinga kujiona na kuongea sana na vyombo vya habari. Mbona Ajibu si kama hivyo?.

    ReplyDelete
  9. kiongozi makini hana mda wa kujibizana na magazeti. Manara unatakiwa ubadilike uwe kiongozi wa timu kubwa kama simba acha uswahili.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic