March 27, 2018


Na George Mganga
 
Kiungo mchezaji wa Simba, Jonas Mkude, aliumia jana wakati kikosi hicho kikijiandaa na mazoezi kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Njombe.

Mkude aliumia wakati akiwania mpira na kiungo mshambuliaji, Mzamiru Yassin na kuepelekea kuanguka chini kisha kutolewa nje ya Uwanja wa Boko Vetarani.

Kufuatia kuumia huko, kwa mujibu wa Afisa Habari wa Simba, Haji Manara, Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, alisema Mkude hajapata maumivu makali, na anaweza akarejea baada ya siku mbili mpaka tatu.

Wakati Simba inajiandaa kuivaa Njombe Mji Aprili 3 2018, kumekuwa na hofu kubwa kwa mashabiki kama ataweza kurejea mapema, japo majibu ya Daktrari yameeleza hatachukua muda mrefu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic