March 27, 2018



Kikosi cha Taifa Stars leo kinashuka dimbani Uwanja wa Taifa kucheza mchezo wa pili wa kirafiki kwa mwaka huu dhidi ya Congo.

Stars inaingia kucheza mechi hii ikiwa na kumbukumbu mbaya ya kupoteza dhidi ya Algeria kwa kipigo cha mabao 4-1 wiki iliyopita.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi, Hemed Morocco, jana alisema maandalizi ya kikosi yameenda vizuri hivyo wamejiandaa kikamilifu ingawa akieleza kuwa mchezo utakuwa mgumu.

Aidha Stars itawakosa wachezaji wawili, Abdulaziz Mohammed na kipa Aishi Manula walio majeruhi.

Mecho hiyo itaanza saa 10 kamili kwenye katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic