March 21, 2018Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino, ameripotiwa kusajiliwa na wababe wa Bundesliga, Bayern Munich, mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa zinaeleza kuwa vinara hao wa Ligi Kuu nchini humo wanaweza wakamsajili Kocha huyo ili kuchukua nafasi ya Jupp Heynckes ambaye ametangaza kustaafu kufundisha soka pale msimu huu utakapomalizika.

Heyneckes alichaguliwa kuinoa Bayern mapema baada ya kuachana na alieyekuwa Kocha wa timu hiyo Carlo Ancelloti mwezi Oktoba mwaka 2017.

 
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV