March 21, 2018


Mshambuliaji wa Atletico de Madrid, Antoine Griezmann, ameitaka klabu yake kutoa mustakabali wa maisha yake ndani ya timu hiyo.

Griezzman ametoa kauli hiyo kutokana na tetesi mbalimbali zinazoeleza kuwa anahitajika FC. Barcelona.

Mfaransa huyo ameeleza kuwa, imefikia wakati sasa anataka kuwa na amani ya kuwa sehemu moja ama nyingine, kuliko kuendelea kusalia njia panda huku hatma yake ikiwa haieleweki.

FC, Barcelona inatajwa kama klabu inayohitaji huduma ya mchezaji huyo ambaye ni tegemeo ndani ya Atletical.

Uwepo wa tetesi hizo, zimemlazimu auombe uongozi wa timu yake kutoa mwafaka juu yake kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic