March 4, 2018


Na George Mganga

Baada ya mvua kupelekea kukatisha mchezo wa Tanzania Prisons dhidi ya Mbao FC katika Uwanja wa Sokone jijini Mbeya, mechi hiyo iliendelea leo kwa dakika zilizosalia na wenyeji kwenda kifua mbele kwa bao 1-0.

Mechi hiyo haikuweza kuendelea jana kutokana na mvua kubwa iliyonyesha na kuepelekea mchezo huo kuahirishwa katika dakika ya 50 ya kipindi cha pili cha mchezo.

Bao pekee lililofungwa na Mohammed Rashid kwa njia penati limeweza kudumu baada ya dakika zote zilizosalia kumaliziwa leo hakukuwa na bao.

Rashid alifunga bao hilo katika dakika ya 11 ya mchezo.

Mbali na mchezo huo, Lipuli FC nao waliikaribisha Ndanda FC na kuweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Mabao ya Lipuli yamefungwa na Mohammed Salamba katika dakika ya 16 na 64, huku bao la Ndanda likifungwa na Nassoro Kapama dakika ya 21.

Mchezo mwingine uliopigwa jijini Mbeya leo uliwakutanisha Mbeya City dhidi ya Mwadui FC, na mpaka dakika 90 zinamalizika, matokeo yalikuwa ni 0-0.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic