March 4, 2018






Na George Mganga
 


Kocha Arsene Wenger amezidi kuongeza presha ndani ya timu yake baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Brighton FC.


Kichapo hicho kimekuwa cha mara ya kwanza kwa Arsenal tangu ifungwe mwaka 1982, imechukua miaka 36 sasa.

Magoli ya Brighton Hovers yamefungwa na Dunk (7') pamoja na Murray (36'). Mpaka dakika 45 za kwanza zinamaliza Arsenal ilikuwa imelala kwa mabao 2-1.

Nyota Pierre Emerick Aubameyang alifunga bao pekee dakika ya 43 kuelekea mwishoni wa kipindi cha kwanza na kuufanya mchezo uende kwa mabao 2-1.

Matokeo hayo yanaifanya Arsenal isalie na alama 45 katika nafasi ya 6.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic