March 21, 2018


Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa, amesema jarida lao linalotoa habari kuhusiana na klabu limesitishwa kwa muda.

Hivi karibuni Yanga ilianzisha jarida hilo mahususi kwa kutoa habari mbalimbali kuhusiana na klabu, lakini kwa sasa halipo tena sokoni.

Kwa mujibu wa EFM Radio kupitia Sports HQ, Mkwasa amesema sababu kubwa iliyosababisha wakasimamisha utoaji wa habari kupitia jarida hilo ilikuwa ni kuangalia soko kama litakuwa zuri kwenye manunuzi.

Aidha, Mkwasa ameongeza kwa kusema wamesitisha kwa muda na watakapokuwa tayari watajipanga tena siku nyingine japo kwa sasa Wanayanga wanaweza wakapata habari kupitia ujumbe mfupi wa maneno 'SMS' kwa njia ya simu.

Yanga wametambulisha huduma hiyo jana ambapo mashabiki wataweza kupata habari motomoto kupitia mtandao wa TIGO.

Huduma hiyo ina tozo la kiasi cha shilingi 100 tu, na ili mtu aweze kujiunga, anapaswa kuandika neno YANGA kisha anatuma kwenda namba 15501.

1 COMMENTS:

  1. walaanza kulitoa kabla awajafanya marketing na promotion

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic