March 27, 2018




Katibu Mkuu wa klabu ya Yanga, Charles Boniface Mkwasa, ametoa maoni yake kuhusiana na na ratiba iliyotoka jana ya mechi zilizosalia kuelekea kumaliza mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mkwasa amesema ratiba imekuwa si rafiki kutokana na baadhi ya mechi kutopishana kwa muda ambao unaweza ukapunguza gharama kutokana na miundombinu ya nchi namna ilivyo.

Katibu huyo ameeleza kuwa ratiba hiyo ni ngumu ukizingatia Yanga pia inashiriki mashindano tofauti na ligi ikiwemo Kombe la FA pamoja na Kombe la Shirikisho Afrika.

"Kwakweli ratiba imekuwa si rafiki ukiangalia kuna baadhi ya mechi inatakiwa twende Mbeya mara mbili, sasa hii inaongeza gharama kwa timu na miundombinu ya nchi yetu ni tatizo" amesema Mkwasa wakati akizungumza na Sports HQ ya EFM.

Hata hivyo, Mkwasa amesema watashirikiana na TFF kuifanya ratiba hiyo iweze kurekebishwa ili kuwapa nafasi ya unafuu kutokana na namna ilivyo hivi sasa.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic