March 24, 2018


Uongozi wa Njombe Mji FC umesema haujapokea taarifa yeyote kuhusu mabadiliko ya terehe mchezo dhidi ya Simba kupangwa kucheza Aprili 3 2018.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Njombe Mji, Hassan Macho, amesema kuwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari, mpaka sasa hazina uthibitisho wowote.

"Kanuni ya ligi kuu inatamka kwamba taarifa za mabadiliko ya mchezo zitatolewa kwa klabu siku 14 kabla ya mchezo husika. Timu ya Njombe mji haijapokea taarifa kuhusu mchezo huo kuchezwa tarehe 3.4.2018" ameeleza.


"Hii itakuwa njia ya kutuondoa kwenye ligi, haiwezekani tukacheze Shinyanga siku mbili halafu turudi Njombe kisha turudi tena Shinyanga siku mbili baadae. Kanuni inataka tupate taarifa siku kumi na nne leo hata tukipewa kesho basi siku hizo hazikidhi kwa mujibu wa kanuni" amesema Macho.

Timu hiyo kwa sasa inajiandaa na safari kuelekea Shinyanga kwa michezo miwili dhidi ya Stand United.

Ratiba iliyopo mpaka sasa iko hivi

Stand United vs Njombe Mji (Machi 30 2018)
Kambarage Stadium
Shinyanga
Kombe la FA

Stand United vs Njombe Mji (April 8 2018)
Kambarage Stadium
Shinyanga
Ligi Kuu Bara


Mbao vs Njombe mji (Aprili 11 2018)
CCM Kirumba
Mwanza
Ligi Kuu Bara


Azam FC vs Njombe Mji (April 15 2018)
Chamazi Complex
Dar es Salaam


Baada ya ratiba hiyo, Njombe Mji itarejea nyumbani mjini Mjombe kucheza na Ndanda FC.

Kwa maelezo hayo Njombe Mji FC inawaomba kupuuza taarifa hizo zisizokuwa rasmi huku ikijikita katika mikakati ya kupata matokeo kwenye mechi za ugenini kama zilivyoorodheshwa hapo juu.
 

Aidha, uongozi huo umesema TFF waiamulie jambo moja la kuitoa kwenye FA au Ligi Kuu.

2 COMMENTS:

  1. Kuliko wajitoe wao wasije watu wapewe point 3.. Wabak kwenye ligi na wabak Fa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic