WAZEE WA NDOMBOLO YA SOLO KUTUA KESHO TANZANIA KUKIPIGA NA STARS ILIYOJERUHIWA
Kikosi cha timu ya Taifa ya Jamhuri ya Kidemorasia ya Congo, kinatarajia kuwasili nchini kesho Jumapili.
Timu hiyo inakuja kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA dhidi ya Taifa Stars, utakaopigwa Machi 27 2018, Jumanne ya wiki ijayo.
Congo inakuja kucheza na Taifa Stars iliyojeruhiwa kwa kichapo cha mabao 4-1 jijini Algiers huko Algeria.
Mechi hiyo itakuwa ya pili kwa Taifa Stars kujipima nguvu na endapo itapata matokeo itakuwa imejitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu kupanda kwenye viwango vya ubora wa soka duniani.
Mpaka sasa, Congo wameshika namba 89 kwa ubora wa soka duniani huku Tanzania ikiwa namba 146
0 COMMENTS:
Post a Comment