March 24, 2018



Unaijua hii? Unaambiwa thamani ya uwekezaji ndani ya klabu ya Singida United inayoshiriki Ligi Kuu Bara ni ndogo kuliko kiasi cha pesa walichokitumia Simba kwenye usajili wa wachezaji wa ligi msimu huu.

Jana wakati Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, akihojiwa kuhusiana na taarifa ambazo zimekuwa zikisambazwa juu ya timu yake bila kuwa na uhakika, alisema watu wasiitumie Singida kama kitu cha juu juu tu.

Aliongeza kwa kusema, ama kuna taarifa ambazo hazina uhakika zimezuka ndani ya klabu watutafute sisi viongozi tutazungumza wapate uhakika, na si kuandika uzushi.

Akihojiwa na Radio One, Sanga alisema kikosi hicho kina thamani ya Bilioni 2.5 hivyo watu wasiichukulie timu hiyo kama sehemu ya mzaha.

Thamani hiyo inakuwa tofauti zaidi na ile ya Simba, ambapo wekundu hao wa Msimbazi walifanya usajili wa kikosi kizima kabla ya msimu huu wa 2017/18 kuanza kwa kutumia kiasi cha pesa bilioni 3.1

Simba ilitumia fedha hicho kwa ajili ya kukiboresha kikosi chao na lengo kubwa ikiwa ni kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic