March 17, 2018




Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Port Said, Misri, ambapo mechi ya Al Masry dhidi ya Simba SC imeenda suluhu ya 0-0.

Matokeo haya yanawapa faida wenyeji, kusonga mbele mpaka hatua ya makundi huku Simba ikitupiwa virago, baada ya mchezo wa kwanza uliofanyika Tanzania kumalizika kwa sare.

Al Masry walilazimisha sare kwenye mchezo wa kwanza kwa jumla ya mabao 2-2, na kuwafanya wawe na faida ya bao moja la ugenini.

Ilitarajiwa Simba wangeungana na Yanga kwenye mashindano haya baada ya suluhu waliyoipata dhidi ya Township Rollers ya Botswana.

Yanga imesalia kama mwakilishi pekee kutoka Tanzania iliyo kwenye mashindano ya kimataifa, kutokana na Simba kuondoshwa na Al Masy.


3 COMMENTS:

  1. Nawatupia lawama makocha kwa kudefend muda mwingi wakati timu hii inafungika tuu..utaona baada kuanza kushambulia mwarabu alichanganyikiwa na kuanza kujiangusha.. vipi kama tungeanza hivyo dk ya kwanza!! Makocha kiukweli wametuangusha wapenzi wa simba!!

    ReplyDelete
  2. Kiujumla simba haieleweki ilemechi hakukua nahaja yakuogopa nawala simchezo wa kusomana ule ulikua ni mchezo wa kutafuta matokeo.mogela,chama,malota,athumani china,George masatu.mohamedi mwameja nawengine wengi ambao sikuwataja.mawazo yangu watumike hawa watu kama wapo hai kuvipa darasa vilabu vyetu kuwa na moyo wakujituma.naona umefika wakati tff kutumia busarazao hao walio liletea taifa faraja hukonyuma.nakama watashindwa niombe wadau wamichezo tukutane ili kushinikiza hawa watu watumike kuwapa moyo vija wetu.nimengi yakuchangia ila pakutolea sauti sina

    ReplyDelete
  3. Kuzungumza na kutupia lawama ni kitu rahisi sana kwa mtu wa kawaida asiejua mpira. Binafsi Simba na viongozi wao pamoja na makocha ni wa kupongezwa sana kwa juhudi walizozionesha katika kuiandaa timu mpaka hatua ya mwisho. Kwa kiasi fulani Benchi la ufundi la Simba linastahili pongezi kwani mipango yao ilifanikiww isipokuwa mechi kama ile Simba ilihitaji mchezaji wa akiba mwenye uwezo mkubwa wa kuusoma mchezso na kufunga ambae angefichwa katika mchezo wa awali na kuwa kama surprise katika mechi ya marudiano. Ukiona timu katika ukanda wetu huu wa Africa inauwezo wa kwenda kuifunga club ya Zambia goli nne mtungi ujuwe hiyo timu sio ya kawaida. Simba wamepambana wanastahili pongezi. Wachezaji wote mnastahili pongezi sana mmeonesha uzalendo hongereni sana. Watanzania imekuwa tabia yetu kuwaingilia makocha katika maamuzi yao na ni moja ya sababu iliyotufikisha hapa tulipo. Simba na Yanga wamekuwa wakipoteza makocha wengi wa maana kwa sababu tu kuna watu wanataka kuwapangia makocha wachezaji wa kuwachezesha. Lakini pia tusisahau pia upumbabu wetu sisi watanzania jinsi Almasry alivyopewa ushirikiano wa kimikakati na baadhi ya watanzania jinsi gani ya kwenda kuimaliza simba pale uwanja wa taifa. Kwanini hatuzungumzii hili kwani kama simba magoli yake mawili yale yangesimama leo tungekuwa tunazungumzia vitu vingine vya furaha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic