STARS INAENDA KUCHEZA NA ALGERIA IKIWA NA KUMBUKUMBU YA KUPIGWA MABAO 9-2, JIKUMBUSHE KIDOGO
Na George Mganga
Kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars, kesho kitakuwa kinashuka dimbani 'Mustapha Tchaker Stadium' huko Blida Algeria kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya wenyeji nchini humo.
Mchezo huo ambao ni wa kalenda ya FIFA, utaifanya Tanzania ipande kwenye viwango vya ubora wa soka duniani endapo itaibuka na ushindi. Hii inachagizwa na ubora walionao Algeria kuwa juu kuliko Tanzania.
Stars inaenda kucheza dhidi ya Algeria ikiwa na kumbukumbu ya kufungwa idadi kubwa ya mabao (7-0) katika Uwanja huohuo watakaoutumia huko Blida.
Kichapo kiliwakuta Taifa Stars wakiwa wanapambania kupata nafasi ya kufuzu kuelekea michuano ya Kombe nchini Urusi mwaka huu.
Mechi hiyo ilipigwa Novemba 8 2015 na kushuhudiwa Waarabu hao wakitawala kila sehemu huku mchezaji Mudathir Yahaya, akilambwa kadi nyekundu kwenye dakika ya 41 tu kipindi cha kwanza.
Mpaka mapumziko Stars tayari ilikuwa imeshalala kwa mabao 3-0.
Magoli ya Algeria yalifungwa na Yacine Brahimi dakika ya 1, Faouzi Ghoulam dakika ya 23 na dakika ya 59 akapachika goli jingine kwa mkwaju wa penati, Riyad Mahrezdakika ya 43 na Islam Slimani kafunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 49 na 75, Carl Medjani dakika ya 72 .
Kwa matokeo hayo Taifa Stars iliondolewa kwenye mashindano hayo ya kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 huko Urusi kwa jumla ya magoli 9-2 baada ya mchezo wa awali kumalizika kwa sare ya goli 2-2 jijini Dar es Salaam.
ilikuwa bahati mbaya kwani kama kawaida hatukuwa na bahati
ReplyDeleteBrother Kwanini unakumbusha maudhi? To be honest hakuna chochote cha msingi cha maana katika suala la ufundi kwenye Timu ya Taifa tangu tupigwe kipigo kile cha aibu. Kwa hivyo wapenzi wa soka tukae tayari kujiandaa na maumivu kutoka kwa Waalgeria.
ReplyDelete