March 21, 2018


Uongozi wa Yanga jana umetangaza kurejea kwa Mshambuliaji wake, Mzibambwe, Donald Ngoma, aliyekuwa majeruhi kwa muda mrefu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa timu hiyo, Hussein Nyika, alisema Ngoma tayari ameshapona na ataanza mazoezi Alhamisi ya wiki hii kujiandaa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United.

Nyika alisema, kwa mujibu wa daktari, mchezaji huyo yuko vizuri kiafya, na kesho Alhamisi atakuwa na wenzake kikosini kuanza mazoezi.

Kuafuatia taarifa hiyo, baadhi ya mashabiki wa Yanga wameanza kuwatambia watani wao wa jadi Simba kutokana na kutangazwa kurejea kwa mchezaji huyo.

Aidha wapo waliofikia hatua ya kusema lazima awatolee cheche katika mchezo utakaowakutanisha watani hao wa jadi kwenye Ligi Kuu Bara.

Mashabiki hao baadhi wa Yanga wanaamini Ngoma anaweza kurejesha makali kwenye safu ya ushambuliaji, wakikumbuka kipindi cha muunganiko wa zamani kati ya Msuva, Tambwe na Ngoma 'MTN'.

Kuelekea mazoezi ya kesho, Yanga itakuwa ina kibarua kigumu cha Kombe la Shirikisho dhidi ya Singida United kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida, Aprili Mosi 2018.

2 COMMENTS:

  1. Yanga msijitambie kwa Ngoma kwasababu yupo njiani kuchotwa na Mnyama

    ReplyDelete
  2. Hata mimi hayo pia nimeyasikia na kuhakikishiwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic