Tim Weah amecheza mechi yake ya kwanza akiwa na timu ya taifa ya Marekani.
Tim ni mtoto wa mwanasoka nyota wa zamani wa Liberia, George Weah ambaye sasa ni raid wa Liberia.
Weah ni Mwafrika pekee kuwa mchezaji bora wa dunia baada ya kushinda tuzo ya Fifa mwaka 1995.
Mwanaye Tim ameichezea Marekani kwa kuwa ni raia katika mechi ya kirafiki dhidi ya Paraguay.
Marekani imeshinda mechi hiyo kwa bao 1-0 na amesema alikuwa akitaka usiku na mchana siku moja acheze timu ya taifa ya Marekani.
Ndani ya mechi tatu, huo umekuwa mchezo wa kwanza Marekani ikishinda chini ya Kocha Dave Sarachan.
Haiingii akilini Mtoto wa Rais wa nchi anashindwa kujitambua wapi alipotoka? Baba na mtoto walikuwa wa kuonesha mfano wa kulipigania Taifa lao la Liberia no matter what kuliko usaliti .
ReplyDeleteNa kesho utashangaa mtoto wa George Weah akichaguliwa kua Rais wa USA!!
ReplyDeleteJe Obama aliisaliti nini Kenya alipochaguliwa kua Rais wa USA !!!
Watu wenye mawazo kama haya ndio wanawanyima haki yao watanzania waliopo nchi za nje kupata dual citizen !!
Tuache ubaguzi sote ni watoto wa Adam na Hawa!!