WATANZANIA MMEOMBWA KWENDA UWANJA WA TAIFA KUWAPA HAMASA NGORONGORO HEROES, KIINGILIO NI BUUREE
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa leo kuipa hamasa timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes.
Ngorongoro Heroes inaingia dimbani kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Msumbiji, mechi ikianza saa 10 kamili jioni.
TFF imewaomba mashabiki na wadau wa soka waende kwa wingi Uwanjani kuwapa hamasa vijana kwakuwa kiingilio kitakuwa ni bure.
Kikosi hicho cha vijana kinacheza mchezo huo ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea kuwania kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika kwa Vijana, chini ya miaka 20 (AFCON U20) dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Machi 31 2018.
0 COMMENTS:
Post a Comment