March 5, 2018


Na George Mganga

Habari njema kwa klabu ya Yanga ni kurejea mazoezini kwa mshambuliaji Donald Ngoma na kiungo Thaban Kamusoko hivi sasa.

Wachezaji hao wameanza rasmi mazoezi ndani ya klabu hiyo, huku Kamusoko akipewa nafasi ya kucheza mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers Jumanne ya kesho.

Ngoma hakuwa na timu hiyo tangu Septemba 2017 kutokana na majeruhi hivyo ameungana na wenzake kufanya mazoezi.

Taarifa kutoka uongozi wa Yanga kwa mujibu wa Kaimu Afisa Habari, Godlisten Chicharito, amesema Kamusoko anapewa nafasi ya kucheza tofauti na Ngoma ambaye ndiyo ameanza mazoezi siku chache zilizopita.

Yanga itaendelea na mazoezi katika uwanja wa Gymkhana uliopo Dar es Salaam leo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic