March 5, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha yanga kinataraji kuendelea na mazoezi jioni ya leo katika Uwanja wa Gymkhana uliopo jijini Dar es Salaam.

Yanga itafanya mazoezi hayo jioni ikiwa ni siku moja kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana.

Mazoezi hayo yatakuwa ni ya mwisho kwa leo kuelekea mchezo huo utakapoigwa siku ya kesho majira ya saa 10 kamili jioni kwenye Uwanja wa taifa.

Ikumbukwe kuwa Yanga ilifuzu kuingia hatua hii baada ya kuwang'oa St. Louis FC ya Ushelisheli kwa jumla ya mabao 2-0.

Wapinzani wao nao walifanikiwa kuwaondoa El Merrikh ya huko Misri.

1 COMMENTS:

  1. Mwandishi Leo umekuwaje mbona kama hauko serious nautowaji wa taarifa yako?hivi ni kweli yanga ilifuzu kwa ushindi wa 2-0?na tounwship iliitoa team ya misr?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic