BAADA YA KUIKACHA MANCHESTER, ZLATAN KUTIMKIA LA MAREKANI
Baada ya Manchester United kutangaza kuvunja mkataba wake, Zlatan Ibrahimovic sasa anahusihwa kuelekea Marekani.
Ibrahimovic amevunja mkataba wa kuendelea kuitumikia klabu hiyo kutokana na hali yake kiafya kutokuwa nzuri na kuepelekea kukosekana Uwanjani kwa muda mrefu.
Taarifa zinazoelewa hivi sasa ni kuwa mchezaji huyo anaweza akaelekea Marekani kujiunga na LA Galaxy inayoshiriki Ligi Kuu nchini humo.
Mshambuliaji huyo alijiunga na Machester United ikiwa mwaka 2016 katika msimu wa majira ya joto akitokea PSG ya Ufaransa, kabla ya kupatwa na majeruhi ya goti la mguu wake Aprili 2017.
Ibrahimovic anaondoka United akiwa ametwaa taji moja pekee la ligi ya Europa.
0 COMMENTS:
Post a Comment