April 25, 2018



Akiwa ana siku moja pekee tangu atue jijini Dar es Salaam, Kocha Mkongomani wa Yanga, Mwinyi Zahera, ameizungumzia kiufupi mechiya watani itakayopigwa Aprili 29 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kocha huyo ambaye amewasili jana nchini akitokea Congo, amesema kuwa hana hofu na watani zake wa jadi, Simba walio vinara kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na alama 59 mpaka sasa.

Zahera ameeleza kuwa yeye ni mzoefu katika soka hivyo hana wasiwasi wowote kuelekea mtanange huo wenye msisimko wa aina yake.

Tayari Zahera ameshawasili mjini Morogoro baada ya kuondoka mapema jana baada ya kumalizana na Yanga.

Zahera yuko Morogoro hivi sasa ili kutia nguvu kwenye kikosi chake kipya kwa ajili ya mechi hiyo dhidi ya Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic