KAULI YA SALUM MBONDE KUHUSIANA NA MECHI DHIDI YA WATANI WA JADI YANGA
Beki wa klabu ya Simba, Salum Mbonde, amesema kuwa wanaendelea kujipanga kuelekea mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga itakayopigwa Uwanja wa Taifa.
Beki huyo ambaye amekosa mechi nyingi msimu huu kutokana na kuwa majeruhi, amesema mechi hiyo itakuwa si nyepesi wala ngumu, kwani atakayejipanga atapata matokeo.
Mbonde ameeleza kuwa mechi inayokutanisha timu hizo za Kariakoo inakuwa ni ya aina yake na si rahisi kutabirikakama wengi wanavyozania.
Akizungumza kupitia kipindi cha Spoti leo cha Radio, Mbonde alieleza ana shauku kubwa ya kucheza mechi hiyo itakayopigwa Aprili 29 2018.
Simba na Yanga zote zipo Morogoro hivi sasa kujiandaa na mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment