April 15, 2018



Arsenal imeshindwa kuendelea furaha ya mashabiki wake leo baada ya kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Newcastle United katika Ligi Kuu England.

Arsenal imekumbana na kichapo hicho ikiwa imetoka kufuzu kuingia hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Uefa Europa League kwa kuitwanga CSKA Moscow ya Urusi kwa mabao 6-3.

Mabao ya Newcastle yamefungwa na Perez (29') pia Ritchie (68') huku la Arsenal likifungwa na Lacazette kwenye dakika ya 68.

Matokeo hayo yameifanya Arsenal iendelee kusalia na alama 54 kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa imecheza jumla ya michezo 33 msimu huu.

1 COMMENTS:

  1. Bao la Arsenal lilifungwa dakika ya 14 na Lacazette na siyo dakika ya 68.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic