AZAM WAIOMBA BODI YA LIGI IWAHURUMIE, SABABU NI HII
Baada ya kupoteza mchezo wa ligi dhidi ya Ruvu Shooting uliopigwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi Aprili 13 wiki hii, uongozi wa Azam FC umeiandika barua bodi ya ligi.
Azam wameiandikia barua bodi wakiomba mchezo wao dhidi ya Njombe Mji FC usogezwe mbele ili kuwapa nafasi wachezaji wao kupumzika.
Ratiba ya ligi inaonesha kuwa Azam watakuwa na mchezo leo Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex ambao unapaswa kupigwa saa moja jioni.
Kufuatia mechi yao na Ruvu Shooting kupigwa nje ya ratiba baada ya mvua kubwa kunyesha na kusababisha Uwanja wa Mabatini kujaa maji Alhamis ya wiki hii, mtanange huo ulisogezwa siku moja mbele na kuchezwa Ijumaa.
Kwa mujibu wa Afisa Habari wa Azam FC, Jaffer Idd, amesema wameiadikia barua bodi hiyo kuomba mchezo usichezwe leo kutokana na mkiuko wa kanuni zinazotaka timu icheze baada ya masaa 72.
“Kanuni zinataka timu icheze moja hadi nyingine kwa tofauti ya saa 72, sisi tumecheza Ruvu Shooting Ijumaa Aprili 13 tunatakiwa kucheza mechi nyingine Jumapili Aprili 15 kitu ambacho kipo nje ya kanuni. Kwa maana hiyo wachezaji watakuwa wamepumzika kwa saa 48 tu tangu tulivyocheza na Ruvu Shooting.” alisema.
0 COMMENTS:
Post a Comment