April 15, 2018



Kikosi cha Zesco United jana kimeendeleza wimbi la ushindi katika Ligi Kuu nchini Zambia 'Zambia Super League' kwa kuilaza Power Dynamos kwa mabao 2-1 ikiwa Uwanja wake wa nyumbani, Levy Mwanawasa.

Mabao ya Zesco yalifungwa na Lazarus Kambole aliyeingia kambani mara mbili katika dakika za 49 na 65 huku bao la Power Dynamos likitiwa kimiani na Kelvin Mubanga kwenye dakika ya 6 ya mchezo.

Ushindi huo umekuwa wa pili mfululizo baada ya Kocha George Lwandamina kurejea klabuni hapo ambapo mechi iliyopita dhidi ya Lusaka Dynamos, Zesco iliibuka na ushindi wa bao 1-0 ikiwa ugenini.

Msimamo wa ligi unaonesha Zesco imekata nafasi ya pili ikiwa imecheza michezo mitano nyuma ya Green Buffaloes iliyo mbele kwa mechi moja, ambapo Zesco imejikusanyia alama 13 huku Buffaloes wakiwa na 16.

2 COMMENTS:

  1. Jamani habari hizi zinawaumiza watani wetu. Huyu Mzambia anataka kuonesha kuwa timu ya yanga ni mbovu nasi ya kiasi chake lakini sasa ndio kapata timu ya kunyanyua heshima yake na wala siyo yakumlaza na njaa ya miezi mitatu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic