Ronaldo alipachika bao la kusawazisha katika mchezo huo wa ligi zikiwa zimesalia dakika kadhaa tu mchezo kumalizika na kufanya matokeo yawe 1-1.
Taarifa inaelezwa kuwa Ronaldo huyo wa Mbeya baada ya kurejea kambini alijikutana akiletewa zawadi mbalimbali na mashabiki wa timu yake kama viazi, mchele, vitunguu na fedha kutokana na furaha waliyokuwa nayo baada ya sare hiyo.
Naddo aliisaidia Mbeya City kutopoteza alama mbili muhimu baada ya kila timu kunyakua pointi moja kwenye Uwanja wa Sokoine mjini humo.
Yanga walijipatia bao lao kupitia kwa kiungo mshambuliaji Rafael Daud katika dakika ya 58 ya kipindi cha pili.







0 COMMENTS:
Post a Comment