April 24, 2018



Baada ya kwenda sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, kikosi cha Yanga nacho kimeamua kuweka kambi mjini Morogoro.

Yanga imeweka kambi maalum Morogoro kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya ligi dhidi ya watani wake wa jadi, Simba SC, itakayopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Aprili 29 2018.

Kikosi hicho kimeanza mazoezi yake jana kwenye Uwanja wa Jamhuri ikiwa ni takribani siku tano pekee zikiwa zimesalia kuelekea mechi hiyo inayoteka hisia za watu.

Mbali na Yanga, Simba nao walikuwa wa kwanza kutia miguu mjini humo baada ya mechi yake ya ligi na Lipuli, ambapo inafanyia mazoezi yake kwenye Uwanja wa Chuo Cha Biblia.

Hivyo timu zote hizo, Simba na Yanga, zipo Morogoro hivi sasa kabla hazijakutana kwenye mtanange wa Jumapili ya wiki hii.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic