April 30, 2018



Na George Mganga

Kikosi cha Yanga kinatarajia kuondoka nchini Mei 3 2018 kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi U.S.M Alger utakaopigwa Mei 7 huko Algiers.

Baada ya mchezo wa jana dhidi ya Simba kumalizika, Yanga sasa wanaweka nguvu zao zote kwenye mashindani hayo ili kuhakikisha wanazidi kufanya vizuri.

Ikumbukwe hivi sasa Yanga ndiyo timu pekee inayoi\wakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo ya kimataifa baada ya Simba kuondoshwa na Al Masry SC kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Habari wa Yanga, Dismas Ten, ilisema kuwa Yanga wataondoka nchini kupitia Dubai ili kuwawahi wapinzani wao mapema kwa ajili ya kibarua hicho.

Yanga ilipangwa kundi moja 'KUNDI D' na timu za U.S.M Alger, Rayon Sports na Gor Mahia FC kwenye hatua ya makundi baada ya kuindosha Wolaita Dicha SC ya Ethiopia kwa jumla ya mabao 2-1.

1 COMMENTS:

  1. Shime Yondani usije ukawatemea mate huko ugenini. Huyu Yondani mimi nikimhisi mtu mtulivo wa kuheshimika sana lakitendo alichokifanya jana si cha kistaarabu. Kipigo katika mashindano ya michezi lazima kitokeo ama kushinda au kushindwa ndio makusudio na bila ya hayo hakuna haja ya michezo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic