April 30, 2018



Mlinda mlango wa zamani wa Simba, Mohamed Mwameja, ameeleza furaha yake kutokana na timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga.

Mwameja aliyewahi kung'ara na kikosi hicho cha wekundu wa Msimbazi miaka ya nyuma na kujiwekea rekodi ya kuwa mmoja wa makipa bora kwenye soka la Tanzania hapa nchini, amefurahi ushindi huo akisema Simba walikuwa na kikosi kipana.

Mbali na furaha ya ushindi, Mwameja ametaja sababu iliyowaangusha Yanga dhidi ya Simba jina ni majeruhi walionao kwenye kikosi chao.

Kipa huyo wa zamani ameeleza kukosekana kwa baadhi ya wachezaji kama Donald Ngoma, Thaban Kamusoko, Amis Tambwe ambao ndiyo mhimili wa timu kumesababisha kikosi cha Yanga kuwa dhaifu kwenye mchezo wa jana.


2 COMMENTS:

  1. Simba ilishawah kucheza ikiwa na wacjezaji wadogo sn yanga wanapataga tabu. Ilishamchezesha manyika timu ikiwa na majeruh tukatoa droo . hvy yanga wanapaswa kujiangalia na kukubali walifungwa

    ReplyDelete
  2. Kwa maana hiyo Yanga ina wachezaji wangapi ambao imesajili kwa ajili ya msimu huu? Mbona akina Ngoma, Kamusoko, Tambwe tu mbona kwingine wanashinda?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic