April 6, 2018




Mshambuliaji nyota wa Simba, John Bocco 'Adebayor' amesema kuwa hakuna kitu kingine kitakachowanyima kwenye msimu huu wa Ligi Kuu Bara zaidi ya mshikamano kwa viongozi, wachezaji, wanachama na mashabiki wa timu hiyo.

Kauli hiyo aliitoa akitoka kuwafunga Njombe Mji mabao mawili pekee huku akifanikisha ushindi wa mabao 2-0 walioupata kwenye Uwanja wa Sabasaba, Njombe na kufanikisha kuiacha Yanga huku wakiendelea kukaa kileleni kwa jumla ya pointi 49.

Mshambuliaji huyo mwenye mabao 12 sawa na mshambuliaji wa Yanga Mzambia, Obrey Chirwa alijiunga na timu hiyo kwenye msimu huu wa ligi akitokea Azam FC baada ya mkataba wake kumalizika.
Bocco amesema licha ya ushindi walioupata dhidi ya Njombe Mji lakini ligi bado ni ngumu, hivyo mshikamano unahitajika ili kufanikisha malengo yao ya ubingwa wa ligi katika msimu huu.

Bocco alisema, ubingwa bado upo wazi kwao na wao hawawezi kubweteka kwani yeye na wachezaji wenzake wapo tayari kuipambania timu hiyo hadi mwishoni mwa ligi kwa ajili la kuwapa zawadi ya ubingwa walioukosa kwa muda miaka mitano.

Aliongeza kuwa, hilo linawezekana kwao kwani wana kikosi imara kitakacholeta ushindani na kufanikiwa kupata pointi tatu kwenye kila mechi watakayoicheza bila ya kuidharau aina ya timu watakayokutana nayo usoni.

"Nwaambie Wanasimba wote kuwa tuendelee kushikamana katika kipindi hiki hadi mwisho mwa ligi kwani sisi wachezaji tunafahamu kiu yao kubwa ni ubingwa pekee na siyo kitu kingine.

“Kwani mshikamano ndiyo silaha yetu kubwa kwa kuhakikisha kila shabiki wa Simba anajitokeza uwanjani kwa ajili ya kutusapoti kama unavyofahamu shabiki ni mchezaji wa 12, hivyo ujio wao kutatupa sisi hamasa na kucheza kwa kujitoa.

“Kama unavyokiona kikosi chetu kimekamilika na wachezaji wote malengo yetu sawa ni kuipa ubingwa Simba pekee na siyo kitu kingine ili mwakani tushiriki michuano ya kimataifa,” alisema Bocco.

SOURCE: CHAMPIONI


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic