April 6, 2018




Kocha wa Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, amewatoa hofu Yanga baada ya kusema kuwa kwa jinsi anavyokiona kikosi cha timu hiyo, anaamini kitaibuka na ushindi dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia, kesho Jumamosi.

Yanga na Dicha wanatarajiwa kupambana katika mchezo wa kwanza wa hatua ya mtoano ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar.

Pluijm ambaye wikiendi iliyopita akiwa na kikosi chake cha Singida United alipambana na Yanga na kuibuka na ushindi wa penalti 4-2 kwenye Kombe la FA, aliwahi kuinoa Yanga na kuifikisha hatua ya makundi ya michuano hiyo ya Kombe la Shirikisho msimu wa 2015/16.

Pluijm amesema kuwa ana uhakika Yanga watashinda mechi hiyo kwani wana uwezo wa kuwashinda wapinzani wao hao kutoka Ethiopia kwani mara nyingi timu kutoka nchi hiyo hazina uwezo mkubwa.

“Na hakika timu ya Yanga itashinda mechi yake dhidi ya wapinzani wao kutoka Ethiopia kwani wana uwezo na mbinu zao na staili yao ya uchezaji ni nzuri, pia timu za Ethiopia hazina uwezo mkubwa wa kushinda mechi hii ingawa hawatakiwi kuwabeza,” alisema Pluijm.

2 COMMENTS:

  1. Ili washinde list ni hii
    1. Rostand 2.Abdul 3.Mwinyi 4. Andrew 5. Nadir 6. Kamusoko 7. Kesi 8.Daudi 9.Mahadhi 10. Ajib 11. Gadiel

    ReplyDelete
  2. Ili washinde list ni hii
    1. Rostand 2.Abdul 3.Mwinyi 4. Andrew 5. Nadir 6. Kamusoko 7. Kesi 8.Daudi 9.Mahadhi 10. Ajib 11. Gadiel

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic