April 6, 2018



Washambuliaji wa Yanga Mrundi, Amissi Tambwe na Mzimbabwe, Donald Ngoma wameondolewa katika sehemu ya kikosi kitakachowavaa Waleyta Dicha katika mechi ya kesho.
Wawili hao wameondolewa baada ya kutonesha sehemu walizoumia ambazo baada ya kupona walianza mazoezi.
Dicha tayari iko nchini kuivaa Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho inayotarajiwa kupigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, kesho.

Wachezaji hao walijitonyesha katika mazoezi ya mwisho ya jana yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Kocha msaidizi wa Yanga, Shadrack Nsajigwa amesema wachezaji hao walipona majeraha yao kabla ya kuanza mazoezi hayo na kujitonyesha.



5 COMMENTS:

  1. Ni mwendo wa majanga kwa kwenda mbele, halafu mnataka mashabiki waje

    ReplyDelete
  2. Ili washinde list ni hii
    1. Rostand 2.Abdul 3.Mwinyi 4. Andrew 5. Nadir 6. Kamusoko 7. Kesi 8.Daudi 9.Mahadhi 10. Ajib 11. Gadiel

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  4. hahahaha Mnatudanganya Tuambie Ukweeeli tu

    ReplyDelete
  5. Hao tunajua mgomo bado unaendelea, walipeni mishahara yao kwani
    hata chirwa na shimbishimbi kukosa mikwaju YA penati ni muendelezo wa migomo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic