April 7, 2018




Straika wa Yanga, Obrey Chirwa tayari amerejea nchini tayari kuanza kuitumikia Yanga katika mechi za Ligi Kuu Bara, ikiwemo ile dhidi ya watani wao Simba, mwishoni mwa mwezi huu.

Chirwa alipewa ruhusa ya wiki moja kwenda kwao Zambia kutokana na matatizo ya kifamilia.

Lakini Chirwa amerejea nchini tayari kuendelea na kazi yake baada ya kuwa amemalizana na kilichomrudisha kwao Zambia.

Chirwa hatacheza mechi ya leo ya Yanga dhidi ya Wolayta Dicha ya Ethiopia ya kuwania kufuzu kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kwani ana kadi mbili za njano, hivyo kwa mujibu wa kanuni hatocheza.

Chirwa alipata kadi hizo katika mechi mbili za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Township Rollers ya Boswana.

Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten amethibitiwa kurejea kwa Chirwa ambaye ni tegemeo katika safu ya ushambulizi ya Yanga.

1 COMMENTS:

  1. nadhani AIBU imekushika sana ndugu mwandishi..usiwe unakurupuka kutoa taarifa bila kufanya uchunguzi, swala la kutuambia CHIRWA yupo ZAMBIA KISA SIMBA, halaf muda huohuo unayakana matapishi yako, baada ya kumuona chirwa yupo JUKWAANI ni AIBU KUBWA...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic