April 15, 2018



Na George Mganga

Wakati kikosi cha Yanga kikiondoka alfajiri ya leo kuelekea Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Wolaita Dicha FC, Ibrahim Ajibu na Andrew Vincent 'Dant, ni miongoni mwa wachezaji waliosalia Dar es Salaam.

Wachezaji hao wameshindwa kuungana na kikosi hicho kutokana na kukumbwa na majeraha hivyo kushindwa kusafiri na timu.

Dante aliumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Waethiopia uliopigwa Uwanja wa Taifa na kumfanya akosekane Uwanjani dhidi ya Singida United.

Ajibu na Dante watakuwa wanapata matibabu ili kuwa fiti kuelekea mechi ya watani wa jadi dhidi ya Simba SC itakayopigwa Aprili 29 2018 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Kushindwa kujumuika na wenzao katika safari ya Ehtiopia, kunawapa fursa ya kujiandaa vizuri kuelekea pambano hilo ambalo huteka hisia za wadau na mashabiki wengi wa soka la hapa Tanzania.

Said Mussa pamoja na Ramadhani Kabwili, nao wamesalia nchini kwa majukumu ya kuitumikia Ngorongoro Heroes ambayo inajiandaa na mchezo wa kufuzu kuelekea AFCON dhidi ya Congo.

3 COMMENTS:

  1. Njaa ndio ilizowazuwia wasende. Mchezaji kama Ajib ni Lulu, na shida zikiendelea bila ya shaka uwezo wake utatetereka bila ya ubishi na mpaka sasa inaonesha yanga hajatokea tajiri wakuinusuru kama ilivo Simba

    ReplyDelete
  2. Hahaa kazi maalum kwa Simba

    ReplyDelete
  3. Mbio za vijiti hivyo mkuu,Jana yanga Leo simba baada ya miaka kadhaa yanga tena huu ndo Moira wa bongo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic