April 25, 2018






Unaweza kusema huu ni mwaka wa shida kwa Haruna Niyonzima.

Niyonzima ambaye tokea amejiunga na Simba amekuwa akihaha nje ya uwanja kwa kuwa nje ya uwanja kutokana na kuandamwa na majeraha.

Lakini leo amepata msimu wa kufiwa na dada yake ambaye imeelezwa anaitwa Hawa Sumaya Twizemana.

Niyonzima anatarajia kuondoka kurejea kwao Kigali ili kuhudhuria mazishi ya dada yake huyo.

Maana yake, sasa ataikosa mechi dhidi ya watani wao Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumapili.

Niyonzima hakuwa na uhakika wa kuanza, lakini angeweza kukaa benchi Jumapili kwa kuwa tayari alisharejea uwanjani.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic