April 16, 2018





MUNICH, Ujerumani
LICHA ya kuwa Bayern Munich imeshajihakikishia ubingwa wa Ligi Kuu ya Ujerumani, bado timu hiyo imeendelea kuwa na makali kwa kuitandika Borussia Moenchengladbach mabao 5-1 katika ligi hiyo maarufu kwa jina la Bundesliga.

Mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la nyumbani la wababe hao la Allianz Arena, ulikuwa wa kuvutia lakini zaidi wenyeji ndiyo waliotawala mchezo na kuwa tishio kwa kiasi kikubwa.

Watazamaji wa StarTimes ambayo huonyesha ligi ya Bundesliga, walishuhudia mabao ya Bayern katika mchezo huo yakiwekwa wavuni na Sandro Wagner aliyefunga mawili, Thiago Alcantara, David Alaba na Robert Lewandowski, wakati lile la wapinzani lilifungwa na Josip Drmic.

Kovac alikuwa chaguo la tatu kwa mabingwa Bundesliga
MUNICH, Ujerumani
SIKU chache baada ya Kocha wa Eintracht Frankfurt, Niko Kovac kutangazwa kuwa atakuwa kocha mkuu wa Bayern Munich kuanzia msimu ujao, imefahamika kuwa mkufunzi huyo alikuwa ni chaguo la tatu kati ya waliokuwa wakipendekezwa kupewa nafasi hiyo.

Hayo yamesemwa na Rais wa Bayern Munich, Uli Hoeness ambaye amekiri kuwa waliokuwa chaguo la kwanza ni Thomas Tuchel na mkongwe Jupp Heynckes ambaye kwa sasa anainoa timu hiyo akiwa kama kocha wa muda.
Kovac, 46, atachukua nafasi hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka mitatu huku kukiwa na kelele nyingi juu ya uamuzi wa wababe hao wa Ujerumani kumtangaza kipindi hiki akiwa bado anainoa timu nyingine, ikidaiwa hakuwa sawa, japokuwa Bayern wenyewe wanapinga hilo. Watazamaji wa StarTimes watamshuhudia kocha huyo msimu ujao akiwa na Bayern.


Bolt: Narudi Dortmund kufanya majaribio
SYDNEY, Australia
BINGWA mara nane wa mbio za michuano ya Olimpiki katika medali ya dhahabu, Usain Bolt amewafurahisha mashabiki wa Borussia Dortmund baada ya kutoa kauli kuwa anarejea klabuni hapo.

Raia huyo wa Jamaica alifika klabuni hapo wiki chache zilizopita na kufanya mazoezi, lakini amesema kuwa anarejea na atakuwa klabuni hapo kwa wiki tatu akifanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Bolt ambaye anasifika kwa kuwa na kasi kubwa ya kukimbia ana umri wa miaka 31 amesema kuwa nia yake ni kuendelea kuwa klabuni hapo kwa muda mrefu zaidi.

“Ni dili kubwa, wengi wanajua nafanya utani lakini kwa sasa niko makini na sitanii, nitarejea Dortmund wiki chache zijazo ili waone vizuri uwezo wangu, wajue kiwango changu na kuona kama nitaweza," alisema Bolt alipokuwa nchini Australia. Kama kweli atasajiliwa, watazamaji wa StarTimes watamshuhudia msimu ujao katika king’amuzi hicho.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic